-->

Wasanii Wanatubania Kwenye Pesa- Jengua

MOHAMMED Fungafunga ‘Jengua’ amefunguka kuhusu wasanii wakongwe kutengwa na wasanii vijana katika masuala yanahusu fedha katika mialiko mbalimbali hasa ile yenye pesa kwa kualikana wao kwa wao japo katika mialiko hiyo wahusika huwahitaji wao na wasanii hao ujibu kuwa wao wapo bize.

jengua

“Tabia za baadhi ya wasanii hawa vijana zinatukera sana sisi wasanii wazee au niseme wakongwe kwani mialiko mingi wanapeana wao kwa wao hasa ile ya hela lakini ya bure wanatuita kwa fujo, si tabia nzuri kabisa,”alisema Jengua.

Mzee Jengua anasema kuwa kazi zisizo na maslahi ndio wanapenda kuwahita na kutumia nguvu nyingi kuwatafuta namba zao wanakuwa nazo lakini katika mipango ya fedha ujifanya wamepoteza nambari za simu zao, hivyo anawashauri wasiwabanie katika kazi na mialiko ya kifedha.

Filamu Central

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364