-->

Wasanii wa Singeli Wananiponda- Msaga Sumu

Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kudai wasanii wengi wa singeli wanatapotea katika muziki kwa sababu ya kutokuwa na heshima kwa watu wanaowazunguka kwenye kazi zao.

Msaga Sumu amebainisha hayo kupitia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE (FNL) kutoka EATV baada ya kupondwa kwa maneno makali kwa kipindi kirefu na wasanii wenzake huku wengine wakimwambia hajui lolote katika muziki huo anaouimba.

“Wasanii wa singeli mimi naamini wananiponda sana, tena nikikaa kimya hivi ndiyo wanasema nimefulia kabisa, kumbe mwenzao huwa najitungia sheria zangu huku nikiwaangalia wao. Lakini huwa nawaambia ukweli kwamba siku zote kwenye muziki ukiwa na heshima unaweza kufika mbali, kwa kuwa heshima ndiyo kila kitu. Lakini hawa wasanii wa singeli wengi watafeli kwa sababu heshima hawana, wanajifanya wanavimba kutokana na nyimbo zao moja moja walizokuwa nazo”, amesema Msaga Sumu.

Mtazame hapa chini Msaga Sumu akifunguka kuhusu wasanii wanaomponda pamoja na mambo mengine.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364