-->

Wastara Afunguka Kuhusu Kuwa na Ujauzito

Msanii wa bongo movie Wastara Juma apinga mawazo ambayo watu wamekua wanamfikiria kwamba ni mjamzito.

Wastara78

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz kinacho onyeshwa katika runinga ya EATV kila siku saa kumi na mbili, Wastara amewaambia wananchi kwamba tumbo la mimba hukua na halirudi ndani kwa hiyo waendelee kusubiri miezi tisa mpaka itimie kwani kwanzia waanze kusema yeye ni mjamzito ni miezi mine na tumbo haliendelei.

Licha ya hilo Wastara amesema tumbo hilo ambalo walikuwa wanalihisi kuwa ni kijacho, ni kwamba aliridhika tuu na sehemu ambayo alikuwa, kwani alikuwa Msumbiji kibiashara kwa hivyo mazingira hayo yalimfanya kuwa na tumbo kubwa na hivi sasa yupo kwenye diet ili kupunguza mwili.

“Unajua kinachonishangaza ni pale wale wanaposema mimi ni mjamzito na haelewi baba kijacho ni yupi kama ni yule wa ndoa ama ?,” alisema Wastara Juma.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364