-->

Wastara Atoboa Sababu ya Kuacha Wanaume

Msanii wa filamu, Wastara Juma ameweka wazi sababu kubwa ambayo ilimpelekea kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Bondi Bin Salim na kwenda kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kisha kuachana naye na kurudiana tena na mpenzi wake

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha (EATV) Wastara anasema aliamua kuachana na Bond kutokana na tabia yake ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi na pombe pamoja na tabia zingine ambazo yeye alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana naye.

Wastara Akiwa na Bond

“Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpka Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi, mpka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi, kwanza kwenye mahusiano kulikua hakuna uaminifu kabisa, ilifikia hatua mpka kuna watoto wengi sana walikuwa wanaletwa wengine ni kweli wengine wa uongo vile vitu binafsi kama mwanamke vilikuwa vinaniumiza” alisema Wastara

Mbali na hilo Wastara anasema baada ya hapo familia yake ilimshawishi aweze kuolewa na Mbunge huyo Sadifu ambaye alikuwa anahitaji kuwa naye na kusema aliwasikiliza sababu siku zote familia yake huwa inaiweka mbele na kuwasikiliza na kuamua kwenda kuolewa na Mbuge lakini anasema baada ya kuingia huko alikutana na matatizo mara kumi ya alipotoka hivyo ndoa hiyo ilimshinda ndani ya siku sabini na kitu  na kuamua kuachana naye.

Wastara alizidi kuelezea kuwa baada ya hapo Bond alirudi toka reharb akiwa ameachana na tabia zake zile na alijiridhisha kuwa sasa amebadilika hivyo akarudiana naye na wanaendelea kuishi pamoja mpka sasa kama wapenzi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364