-->

Water Chilambo Aomba Nyimbo Zake za Bongo Fleva Sizipigwe,Wamsapoti Kwenye Gospel

Aliyekuwa mshindi wa BSS Water Chilambo amesema anaomba TV na Radio kuacha kupiga nyimbo zake za bongo fleva kwa sasa na wamsapoti kwenye muziki wa Gospel ambao anaufanya.

Water Chilambo

Akipiga story kupitia eNewz Chilambo amesema wametokea wasanii wengi pamoja na waandaaji wa muziki kumuita ili waweze kufanya kolabo ya nyimbo ya bongo fleva lakini aliwakatalia hali iliyowapelekea wengine kutokumuamini na kuhisi kwamba anaringa.

Lakini pia Chilambo amesema ameamua mwenyewe kubadilika na kuingia kwenye nyimbo za injili na kumtumikia Mungu na hakuna shida yoyote aliyoipitia wala hajashauriwa na mtu yeyote kuingia kwenye nyimbo za injili bali alijikuta tu mwenyewe anaingia kwenye muziki wa injili na kuupenda zaidi.

Hata hivyo Chilambo hakusita kusisitiza na kuwaambia wasanii wenzake kwamba “Siwezi kumridhisha kila mtu bali namuangalia Mungu wangu sitaweza kuingia kwenye akili za watu kuwaambia kwa sasa nafanya muziki wa injili hivyo nawasihi wasanii wenzangu pamoja na media kunisapoti huku kwenye muziki wa injili kwani nimeamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kutoka moyoni na siyo vinginevyo”.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364