-->

Wazazi Walimkataa Alienipa Ujauzito-Linnah

Msanii wa muziki Linah Sanga ambaye kwa sasa ni mjamzito amefunguka kwa kudai kuwa wazazi wake walimkataa mpenzi wake wa sasa kwa kigezo cha dini.

Muimbaji huyo ambaye amelelewa katika misingi ya dini ya kikristo, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa haikuwa rahisi kwa wazazi wake kumkubali mwanaume huyo.

“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi,” alisema Linah. “Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti,”

Aliongeza, “Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.”

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Mfupi’ aliouachia hivi karibuni.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364