Wema Sepetu Ampa Makavu Harmorapa
MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu, ‘Madam’ amemfungukia Msanii wa Bongo Fleva, Harmorapa baada ya hivi karibuni kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kumuoa Wema.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram, Wema ameandika kuwa anamheshimu Harmorapa kama msanii mwenzie hivyo kitendo cha kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kuwa na Wema katika mahusiano si sawa ajaribu kwa watu wengine na si yeye.
Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe…. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*
Wema ameandika.