-->

Waziri Nape Akutana na Wasanii wa Bongo Movie

Waziri Nape akito ufafanuzi wa jambo.

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekutana na wasanii na wadau wa tasnia ya filamu nchini kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu tasnia hiyo.

waziri-nape-nnauye-9

Katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar, wasanii na wadau wa filamu wamelalamikia suala la wizi wa kazi zao ikiwemo urudufishaji, kuuzwa holela huku wahusika wakiendelea kupata hasara na watu wengine (wezi wa kazi hizo) kujinufaisha wenyewe.

waziri-nape-nnauye-8Mwigizaji, Bi Mwenfda akiuliza swali kwa wazri Nape.

Akijibu hoja hizo, Nape amesema kuwa serikali ya Awamu ya Tano inatambua mchango wao na changamoto zinazoikabili tasnia ya filamu hapa nchini, atahakikisha anazishughulikia changamoto hizo kwa kushirikiana na wasanii weneyewe ili kuinua na kuikuza zaidi tasnia hiyo.

waziri-nape-nnauye-7

Ikumbukwe kuwa, miezi kadhaa iliyopita, Waziri Nape alifanya ziara ya kushtukiza katika maduka ya CD na DVD, Kariakoo jijini Dar na kukamata shehena ya CD na DVD feki.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364