Wema Awapa Makavu ‘Team Wema’
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amewatimua watu wanaojiita Team Wema waliotapakaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, akisema hawataki kwa vile wanamharibia maisha yake.
Katika sauti aliyoituma katika akaunti ya mtandao wake wa Instagram, alisema haelewi hasa asili ya watu hao kujihusisha na jina lake, lakini anakerwa zaidi nao kwa kitendo chao cha kutaka kuingilia maisha yake binafsi, ikiwa ni pamoja na kumshambulia mama yake.
“Siwajui hawa watu na sijui walikotokea, nasema siitaki hiyo team Wema kwa sababu hainisaidii lolote, kama ni huyo Idriss endeleeni naye, sitaki kusikia kabisa, hawana mchango wowote kwani, hao ni wanafiki na mimi katika maisha yangu sitaki unafiki, mimi ni mtu wa wazi, sitaki,” alisema msanii huyo.
Kukiwa na sauti zinazoonekana kumpunguza jazba mrembo huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema hakukubali, bali aliendelea kutoa maneno makali akiwashutumu watu hao, ambao kwa muda mrefu, wamejitambulisha kama mashabiki wake wanaopambana kwa nguvu kubwa na wapinzani wake kisanaa.
Chanzo:GPL