-->

Wema Sepetu abadili uamuzi wa kung’oa kizazi

Mwigizaji Wema Sepetu anaonekana kuyatafuna maneno yake ya awali, alipokiri kwamba atatoa kizazi chake kama hatakuwa amefanikiwa kushika mimba atakapotimiza miaka 32.

Kwa kipindi kirefu, Wema mwenye miaka 29 amekuwa akihangaika kupata mtoto bila ya mafanikio. Mwaka jana alipokuwa na uhusiano na mshiriki wa zamani wa Big Brother Idris Sultan, alieleza kwenye mitandao ya kijamii kuwa alishika mimba lakini ikaharibika.

Wema alisema, “Nampenda mtoto nipate mtoto hata sasa hivi, kwa sababu nimekuwa nikitaka tangu nina miaka 24 sasa hivi nina miaka 29. Kwa kweli hali hii inaniumiza kila leo. Lakini nasema kwamba sijakata tamaa, Mwenyezi Mungu najua ana mipango yake na ukikataa sana tamaa pia unamkufuru.”

Lakini licha ya kukosa mtoto, mrembo huyo alisisitiza hawezi kukata tamaa na ataendelea kusubiri kwa imani na ipo siku Mungu atasikia kilio chake na atamjalia.

“Mimi ni mtoto wa Kiislamu sitaki itafika mahali nitaanza kumfukuru Mungu. Nina Imani kwamba God’s time is the best time acha tuone. Itakavyokuwa Inshallah,” Wema amesema.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364