Wema Sepetu Afunguka Kuhusu ‘Range’ Yake, Aeleza Kilichotokea
Baada ya kuzagaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya magazeti kuwa ile ‘Range Rover Evogue’ ya staa wa filamu, Wema Sepetu aliyojizawadi katika siku yake ya kuzaliwa imekamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa madai alikwepa kulipa kodi, Wema amesema gari yake ipo nyumbani kwake.
Akizungumza na 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jumatatu hii, Wema alisema baada ya kukamatwa na (TRA) aliwaonyesha document za umiliki wa gari hiyo na baadae kumuachia.
“Gari ni langu, nimelinunua na kitu kilichobaki sasa hivi ni kulisajili tu, lipate namba za Tanzania,” alisema.
“Sasa hivi TRA wapo kila sehemu hata sasa hivi ninapoongea rafiki yangu amekamatwa na gari ina namba za Afrika Kusini. Kwahiyo sasa hivi TRA wanafanya kazi, jamani Magufuli sasa hivi ana Magufulika, kwahiyo tuache wafanye kazi zao. Yeah walinifuatilia, kwahiyo wanafuatilia kila gari ambalo lina namba ngeni. Kwahiyo ukiwa na document za kumiliki hawakusumbui, hapa tunapo ongea gari yangu ipo nyumbani kwangu, walihitaji document nimewapatia ndiyo maana wameniachia.,” alieleza Wema.