-->

Wema Sepetu Afungukia Ishu ya Umri Wake

Msanii wa filamu nchini ambaye pia alishawahi kutwaa taji la mrembo wa Tanzania Wema Abraham Sepetu, amewacharukia na kuwajibu watu wanaoendelea kumsema vibaya kuhusu umri wake sahihi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Wema Sepetu ambaye hivi karibuni amesherehekea siku ya kuzaliwa na kutimiza miaka 29, amesema kama wao ndio wamemzaa basi umri wanaotaja ndio sahihi.

“Hao wanaosema kama wao ndio wamenizaa sawa, lakini aliyenizaa mama yangu Bi Mariam Sepetu ndio anajua umri wangu sahihi, sasa wao wanalazimisha sijui nimezaliwa lini, hawajanizaa wao, walionizaa ni Mariam Sepetu na Dady Isaac Abraham Sepetu sio wao”, amesema Wema Sepetu.

Baadhi ya watu wamekuwa wakisema Wema Sepetu anadanganya umri wake kwa kujipunguzia aonekane mdogo, lakini wao wanadai kwamba msanii huyo ana umri zaidi ya huo anaoutaja, jambo ambalo Wema Sepetu mwenyewe amelipinga na kusema huo ndiyo umri wake sahihi.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364