Wema Sepetu Ataka Mashabiki Waheshimiwe
STAA wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, amesema ni upuuzi kwa msanii kutomheshimu shabiki wake kwa kuwa bila huyo hawezi kuwa msanii.
Wema alisema kwa kuwa msanii ni kioo cha jamii, hivyo hatakiwi kutoheshimu mashabiki wake kwa kuwa hao ndiyo wanaomsaidia kisanii.
“Kuna baadhi ya wasanii wanatumia majina yao vibaya, ukiwa staa unatakiwa uwe ‘smart’ ujipende, uwe na upendo na wenzako, uwe mvumilivu unayejiheshimu na kuheshimu watu wako wakiwamo mashabiki,’’ alieleza Wema.