-->

Wema Sepetu Kujifungua Mwezi August

Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu anatarajia kujifungua mwezi August 2016, kwa mujibu wa mpenzi wake Idris Sultan.

wema56

 

Akizungumza katika kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Jumanne hii, Idris alisema mpenzi wake huyo anatarajia kupata mtoto baada ya miezi 6 au 7 hali ambayo imetafsiriwa na wadau wa mambo kuwa huenda mwanadada huyo akawa na mimba ya miezi 3 au 2.

“Yes very soon natarajia kupata mtoto kama miezi 6 au 7 ijayo,” alisema Idris. Pia Idris alisema bado hajatambua jinsia ya mtoto anayetarajia kujifungua mpenzi wake.

“No hatujui mwenzangu anataka surprise. Mimi nataka kujua kabla kwahiyo bado hatujafikia muafaka, naogopa nisije nikawa nanunua vigauni akaja Wa kiume bure,” alisema.

Aliongeza, “Huwezi kuwazuia watu kuongea, waache waongee maana sometimes watu ni wagumu kupokea changes lakini siku zinavyoenda naamini wataelewa tu.”

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364