-->

Wivu Utaniua – Shamsa

Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford amefunguka na kusema kwamba hataweza kukubali Mume wake kuongeza mke wa pili kama hataweza kumpa sababu maalumu kwa kuwa anaamini anamtosheleza mume wake kwa kila kitu.

Shamsa amefunguka hayo kwenye FNL na kusema kuwa wivu alionao juu ya mume wake hafikirii kama atakubali kirahisi kuongezewa mke mwenza huku akiwa hana matatizo yoyote,

“Wivu nilionao siwezi kukubali kuongezewa mke wa pili hata mume wangu (Rashid) anajua kwa sababu yeye mwenyewe ana wivu sana na mimi. Ukweli kabisa nahisi ninaweza hata kufa kwa presha nikiongezewa mke wa pili. Inabidi kwanza kabisa kabla ya kuniomba aoe, anatakiwa anipe sababu za msingi kwannii anaamua kufanya hivyo na ikiwa sababu zinamashiko na mimi nikazielewa basi nitamruhusu kwa kuwa dini inasema hivyo kwa sababu pia ni ibada. Lakini kama hazina msingi siwezi kukubali kwa sababu naamini namtosheleza kwa kila mtu na sina kasoro yoyote”, Shamsa aliongeza

Pamoja na hayo Shamsa ameweka wazi malengo ya kuongeza mtoto mwingine kwani amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa mwanae ambaye kila siku amekuwa akisisitiza kuomba mdogo kae.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364