-->

Wolper Afungukia Kutokuvaa Nguo za Kiume Kwasasa

Mwigizaji kutoka kiwanda cha filamu bongo, Jacqueline Wolper amesema mchumba wake ndiye sababu iliyomfanya apunguze kuvaa nguo za kiume.

wolper23

Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi nimeshakuwa na mchumba’.

“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.

Wolper aliendelea kusema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”

Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa anafanya.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364