-->

Wolper Hafikirii Kabisa Kujibusti

JACQUILINE Wolper, mmoja ya nyota wa kike wa filamu nchini, ametamba anajiamini kwa urembo alionao wa rangi na sura na kwamba hana mpango wa kujitengeneza.

Wolper alisema kuwa hana muda wa kutumia dawa yoyote kukuza makalio yake au chochote mwilini mwake kama kinadada wengine wafanyavyo kwani anaukubali uumbaji wa Mungu.

“Kuna watu wanajibusti mzee, utaona binti alikuwa na mwonekano wa kawaida lakini ghafla makalio yamekuwa makubwa, sijui matiti yamenona na rangi kubadilika nasikia wapo wanaochoma sindano na kunywa dawa, siwezi,” alisema.

Wolper alisema hajawahi kufanya upuuzi huo na hawezi katu kumtania Mungu kwa sababu anaheshimu uumbaji aliomfanyia kwani yeye ni mmoja ya warembo kweli kweli.

“Weupe wangu ni wa asili na mashallah ni mrembo wa sura na umbo, kwa nini nimkosee Mungu kwa kujibusti, siwezi na nitaringia shepu niliyonayo,” alisema Wolper ambaye ameshiriki katika filamu mbalimbali za Bongo Muvi.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364