-->

Wolper Kaanza Kusakamwa Tena Jamani

WANADAMU hawana dogo kwani wameanza kumsakama nyota wa filamu nchini, Jacqueline Wolper, wakidai amerudia tabia ya kuvaa mavazi ya kiume ambayo yanawakera na badala yake kumtaka avae magauni marefu kwani ndio yanayompendeza.

Wolper ameonekana katika maeneo tofauti akiwa amevalia mavazi hayo ya kiume tofauti na magauni yake marefu ambayo alikuwa akitoka nayo.

Mashabiki wake hao wametoa maoni yao katika akaunti yake ya Instagram wakimsihi asirudie ya zamani kwa kuvaa mavazi ya kiume, kwani hayampendezi na yanasababisha jamii imfikirie vibaya.

Kwa upande wake, Wolper, ameliambia Mwanaspoti anawaheshimu mashabiki hao ila waelewe kuna wakati anahitajika kuvaa mavazi hayo kwani yeye ni mwanamitindo anayetengeneza nguo, hivyo analazimika kuzivaa ili kuvutia wateja wake.

“Kweli maoni yao nimeyapokea vizuri tu, ila inabidi watambue kuwa mimi ni mwanamitindo na mara nyingi nguo hizi huwa natengeneza na kuziuza. Najaribu kuvaa mavazi tofauti ili kuvutia biashara yangu. Hizo picha wanazoziona katika akaunti yangu ni sehemu ya matangazo ya kazi zangu,” alisema Wolper.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364