-->

Young Dee Afungukia Tetesi za Kurudia Unga

Young Dee amejibu kwa ufupi kuhusiana na tetesi kuwa amerudi tena kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

kiandika maneno mafupi sana kwenye post yake mpya ya Instagram, Young Dee amedai kuwa ‘muda utaongea.’

“Time will Tell… Mi sina tatizo na mtu… Tuombeane kheri tu… Siwezi shindana na maneno,” ameandika rapper huyo.

Wiki hii tetesi za kuwa Dee amerejea tena kwenye utumiaji wa dawa hizo zilianza kufuatia maneno ya meneja wake Max mtandaoni. Max alida kuwa rapper huyo ameanza tena kuubwia unga na kwamba amechoka kusumbuka naye.

Tetesi za Young Dee zimekuja katika kipindi ambacho watanzania wanasikitishwa na hali walizonazo Chidi Benz na Nando kutokana na kuathirika vibaya na madawa hayo.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364