-->

Yusuph Mlela Atoa Angalizo Hili kwa Wanaotafsiri Filamu za Nje (VIDEO)

Muigizaji wa filamu za Bongo Yusuph Mlela amefunguka na kudai kwamba wapo tayari kupambana na mtu anayetafsiri filamu za nje kwa lugha ya Kiswahili na kuziuza kwa bei rahisi, ili kunusuru soko la filamu  la ndani lizisije kufa.

Mlela ameongeza kuwa wao kama wasanii wasipoonyesha juhudi za kupigania soko la filamu basi kizazi chao kitakuwa hakijaonyesha juhudi zozote za kupambana na maharamia hao ambao ndio chanzo cha kazi za sanaa za bongo kushuka na kwamba watu hao wanafanya kazi bila kufuata utaratibu.

Mlela ameendelea kufunguka mbele ya kamera za eNewz kuwa zoezi la kumdhibiti mtu anayedurufu kazi za wasanii halijaanza sasa na kwamba muda mrefu  harakati za kumdhibiti mtu huyo zilikuwa zikifanyika ila kwa kuwa zoezi limepatiwa nguvu zaidi litafanikiwa.

Mtazame hapa chini Mlela akifunguka zaidi.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364