-->

Z-Anto Afungukia Ujio Wake Mpya, Ataka Kusainishwa Lakini

Msanii Z Anto ambaye amekuwa kimya muda mrefu kwenye game na kutangaza kurudi hivi karibuni, amefunguka kuhusu kitendo cha msanii kumsaini msanii mwenzake kwenye lebo yake na kufanya naye kazi.

z-anton

Akizungumza kwenye FNL ya east Africa Television na East Africa Radio, Z Anto amesem akitendo hicho kwake ananona ni kitu kigumu kwake, kwani iwapo msanii atamsaini msanii mwenzake kwa hapa bongo, haitakuwa rahisi kumuachia awe juu yake, na badala yake ataendelea kubaki chini yake.

“Kuna dosari nyingi ambazo naziona kwenye hizi lebo za bongo, kila mmoja anataka kumpita mwenzake, Je, atakayenisimamia atakubali nimpite!? Mimi ni mshindani, naangalia kwa nini anafanya vizuri ili kwenye uandishi wangu na kazi zangu nijue nampita wapi”, alisema Z Anto.

Z Anto aliendelea kwa sasa ameshapata ofa za management 8, ambapo 2 kati ya hizo ni kubwa lakini bado hajafanya uamuzi ni ipi ambayo atafanya nayo kazi.

“Nina ofa takriban 8 za management, mbili ndio kubwa lakinibado sijafikia uamuzi, na kama nitakubali itakuwa kwa masharti magumu sana, na nina kila sababu ya kusema masharti yatakuwa magumu kwa sababu nina uwezo wa kufanya kazi”, alisema Z Anto.

Z Antoa alihitimisha kwa kusema kwa sasa amshajipanga vya kutosha na kila kitu kipo tayari kwa ajili ya ujio wake huo, lakini kinachosubiriwa ni video tu.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364