-->

Zuu: Mimi mzuri zaidi ya Shilole

Yule Video Vixen wa ngoma mpya ya Nuh Mziwanda ‘Jike Shupa’ ambaye anafahamika kwa jina la Zuu amefunguka na kusema kuwa yeye ni mrembo zaidi ya Shilole na amejaaliwa kuliko huyo Shilole.

zuu

Zuu akiwa na Nuh Mziwanda

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV Zuu amedai kuwa yeye ni zaidi ya Shilole kwani yeye ni mweupe zaidi wakati Shilole ni mweusi, yeye ana mguu mzuri zaidi na umbo zuri kwani hatumii mchina.

Video Vixen huyo amesema kuwa yeye aliitwa kwenda kufanya kazi na wala hajawahi kumuangalia Shilole nyuma alikuwa anafanya nini, bali alikuta script na kufanya kila kitu ambavyo script ina muongoza kufanya kazi hiyo na ndicho alichofanya mpaka kazi hiyo imetoka na kuwashika watu.

Mbali na hilo Zuu amedai kuwa kwa mara ya kwanza aliwahi kushiriki katika wimbo wa Daz Baba ‘Umba namba nane’ lakini pia ametumika kama video Vixen katika wimbo mpya wa Harmonize uitwao ‘Matatizo’ ila bado haujatoka pamoja na hii Jike Shupa iliyompa umaarufu zaidi.

SHILOLE23

Shilole

 

eatv.tv

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364