-->

Wema Afunguka Kuhusu Kurudiana na Diamond

Vunja ukimya! Tetesi zinazogonga vichwa vya mashabiki wa mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimepata ufumbuzi baada ya mlimbwende huyo kuanika ukweli wa ‘ubuyu’ huo, Wikienda limefanya naye mahojiano maalum (exclusive interview) yaliyochukua dakika 45.

wema012

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ enzi za penzi lao

KABLA YA MAHOJIANO
Kabla ya Wema kufunguka mambo mazito juu ya Diamond, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, sababu hasa za mashabiki wa wawili hao kuhisi penzi lao limefufuka chini kwa chini ni baada ya Wema kuanza kuwahimiza watu kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wampigie kura Diamond ambaye anawania Tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, zitakazofanyika nchini Marekani hivi karibuni.

JIUNGE NA WEMA
Wikienda: Mashabiki wako wapo kwenye sintofahamu ya tetesi za wewe kurudiana na Diamond. Je, ukweli ni upi?
Wema: (kicheko cha kukata na shoka hadi machozi) hivi kwa nini kila ninapokutana na mtu lazima aniulize kuhusu mimi kurudiana na Nasibu (Diamond)?
Wikienda: Sasa hapo ndiyo ujue lisemwalo lipo na kama halipo laja, hebu eleza hili likoje?

Wema: Kwanza kabisa mimi sasa hivi nimekua. Utoto nimeuweka kando, sihitaji tena bifu zisizokuwa na maana na hata ukiangalia ni kitu gani tulichogombania, hakuna hivyo kuna wakati unafika lazima mtu ubadilike kabisa tena kwa kipindi kama hiki cha mwezi mtukufu.
Wikienda: Kuna mtu yeyote alikushauri kuanza kuposti watu wajitoe kumpigia kura Diamond?

Wema: Hakuna, mimi niliongozwa na hisia zangu kwa sababu hata hivyo sipendi kupelekeshwa na hisia za watu au watu wanasema nini, inatakiwa ifike kipindi nifanye vile moyo na akili yangu inavyotaka.
Wikienda: Unajua kuna kitu kinaitwa timu, yaani kati yako na Diamond. Vipi kwa upande wako hawajakujia juu kuhusu kuwataka mashabiki wampigie kura Diamond kwa sababu mara nyingi timu zenu huwa zinatukanana?

Wema: Kwanza hilo ndilo nataka kuliweka wazi, sasa hivi sitaki kuendesha maisha yangu kupitia timu kwa sababu mwisho wa siku mimi nina maisha yangu na wao wana maisha yao, yaani mpaka vitu vingine vinakera kwa sababu mtu unatakiwa kufanya kitu kinachotoka ndani ya moyo wako siyo kusikiliza watu wanataka nini.
Wikienda: Kwa hiyo unaona timu ndizo zinachochea ugomvi wenu?

Wema: Kabisa kwa sababu inatokea wakati anatukanwa Diamond, mtoto wake (Tiffah) na mkewe (Zari) kiukweli naomba kusema wazi mimi sipendi na mara nyingi naonekana kama mimi nimewatuma. Aisee sipendi kabisa hali hiyo na ninaomba timu zipunguze kutukana watu siyo vizuri.
Wikienda: Unafikiri timu imekusababishia matatizo?

Wema: Siyo kwangu tu hata kwa Diamond. Hatuishi maisha ya kwetu, tunafuatisha timu. Labda niseme kwamba mimi ni shabiki namba moja wa nyimbo za Diamond lakini kiukweli hata ukitaka kuimba wimbo unajificha yaani maisha hayo sitaki tena kwa sababu hata nje ya uhusiano wa kimapenzi tuliokuwa nao huko nyuma  mimi ni shabiki mkubwa wa nyimbo zake, sasa kwa nini nibane hisia za kitu nikipendacho?

Wikienda: Kwa hiyo kinyongo ulichokuwa nacho nyuma sasa hivi huna tena?
Wema: Yaani mimi nimesafisha nia kabisa, sina tatizo na yeye kwa sababu najua inawezekana hata yeye anatamani kuniuliza kitu inashindikana au anahitaji kufanya kazi na mimi inakuwa ngumu kitu ambacho ni mambo ya kizamani kabisa.

Wikienda: Mara ya mwisho kuwasiliana na Diamond ni lini?
Wema: Niliwasiliana na Diamond tena kwa kumtumia meseji kipindi f’lani mama yake alikuwa anaumwa. Kiukweli kama mapenzi yalikwisha zamani sana. Yeye akaendelea na maisha mengine na mimi hivyohivyo.
Wikienda: Ukipata nafasi ya kukutana naye ili mfanye kitu kwa ajili ya mashabiki wenu inawezekana?

Wema: Kama nilivyosema awali, kwa upande wangu mimi sina tatizo lakini najua kabisa kuna vitu Diamond anavifanya vibaya kwangu ili kunizibia sehemu f’lanif’lakini sasa hiyo inanionesha nini kwa Diamond? Amekuwa kimuziki lakini siyo yeye mwenyewe, kuna kipindi namuonea huruma sana kwa mambo yake, natamani hata nimwite tukae chini na kumwambia kuwa yeye ni wa kimataifa hivyo mambo ya Kiswahili hayana nafasi tena kwake.
Wikienda: Kwa hiyo mtu akiwakutanisha mzungumze upo tayari?

Wema: Bila tatizo lolote, mambo ya matashititi hayahitajiki kwa sasa na hayana nafasi kwani imefika kipindi watu tumekua na maisha yanaendelea kwa sababu siwezi kumfikiria tena kimapenzi.
Katika mahojiano hayo, Wema alidai kwamba kuna mambo mengi ambayo Diamond amekuwa akimfanyia umafia hivyo tetesi kuwa amerudiana naye hazina ukweli wowote na kwamba haitatokea.

Chanzo: GPL

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364