-->

Abdukiba Atoboa Siri ya Alikiba

Msanii Abdukiba ambaye ni mdogo wa Alikiba ametoboa siri kuwa Alikiba anaweza kuachia ngoma yake mpya pindi atakaporudi Tanzania kutokea nchini Kenya ambapo amekwenda kufanya mambo mawili matatu na gavana wa Mombasa Hassan Joho.

Abdukiba alipoongea na East Africa Radio kupitia kipindi cha PlanetBongo aliweka wazi kuwa Alikiba yupo nchini Kenya na kusema amekwenda kushirikiana na gavana Joho katika baadhi ya  mambo.

“Alikiba yupo japo sasa yupo nchini Kenya amekwenda kufanya jambo na gavana wa Mombasa Joho ila nadhani hawezi kumaliza wiki atarudi nchini, kwa hiyo nachojua mimi yeye yupo kwenye mchakato wa kuachia ngoma mpya hivyo naamini akisharudi kila kitu kitakuwa sawa” alisema Abdukiba

Siku ya Alhamisi Alikiba aliweka ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram akionyesha kuwa jambo ambalo lilimpeleka nchini Kenya kuwa limekamilika na kusema amejisikia furaha na fahari kubadilishana mawazo na kaka zake pamoja na dada zake katika muziki waliopo Mombasa, na kusema aliwashauri wamtegemee sana Mungu, wajiamini wenyewe na mwisho wanapaswa kuwa na nidhamu ili kuweza kufika mbali zaidi.

Alikiba amekuwa akilalamikiwa na mashabiki zake kuwa anachelewa sana kutoa wimbo jambo ambalo yeye mwenyewe alisema siyo kweli kwani kuna nyimbo nyingi za kushirikiana ambazo ametoa katikati, ila akasema kuwa alichogundua watu wanataka kumsikia yeye mwenyewe, hivyo akaahidi kuwa wimbo wake mpya ambao utatoka utakuwa ni wimbo wa kwake peke yake kulingana na matakwa ya mashabiki zake.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364