-->

Nisha Anasa Penzi Jipya, Abadili Jina

MSANII wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amebadili jina lake na kujiita Nisha Minhal Azad huku kisa kikidaiwa kuwa amefanya hivyo baada ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na ‘Serengeti Boy’ anayetumia jina hilo.

Alichokiandika Insta.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na msanii huyo, Nisha amekuwa karibu na ‘Serengeti Boy’ huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva na kwamba ameamua kuanika kabisa uhusiano huo bila kificho.

“Nisha amepata tulizo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na mwanaume. Huyo mpenzi wake wa sasa ni msanii wa Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Minu, yaani Nisha humuelezi chochote juu ya dogo huyo na wanaongozana mara kwa mara,” kilidai chanzo na kuongeza;

“Kwa sasa ameamua kuanika ukweli huo kila kona, kwenye mitandao ya kijamii amebadilisha mpaka jina lake na kujiita Nisha Minhal Azad. Hivi karibuni aliweka picha katika Insta yake akiwa naye katika pozi la mahaba na kuandika; ‘kuna tofauti kubwa kati ya Serengeti na Ngorongoro.’

Baada ya kunasa madai hayo, Ijumaa lilimtafuta Nisha na kumuuliza ukweli juu ya kinachoonekana na kuongelewa, alipopatikana alikiri kubadili jina na kuwa katika uhusiano na Serengeti Boy huyo;

“Ni kweli nipo katika uhusiano na huyo mtu, mengine siwezi kuyaanika ila kifupi ni hivyo.”

Nisha kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elbariki ‘Nay wa Mitego’ pamoja na Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364