Sitegemei Kugombana na Alikiba – Baraka The Prince
Msanii Baraka The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana tofauti yoyote na Alikiba na kudai kuwa watu wa mitandaoni ndiyo wamekuwa chanzo cha kusambaza maneno hayo kuonyesha yeye ana tofauti na Alikiba.
Baraka The Prince amedai kuwa yeye hawezi kugombana na Alikiba na wala hategemei kuja kumkosea kwa kuwa ni moja kati ya watu ambao wanampenda sana yeye pamoja na sanaa yake.
“Unajua ukidili wa watu wa Instgram wanaumiza sana kichwa kwa sababu mimi nipo kwenye label moja na Alikiba, hivyo Alikiba ni brother wangu na naishi naye kama kaka yangu kabisa, pia ni miongoni mwa watu ambao wananipenda sana, hivyo sitegemi kuja kumkosea au hata kugombana naye sitegemi kitu kama hicho, sema watu walianza kuongea hivyo baada ya kuona siongozinaye kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, watu wamezoea kuniona kila anapokwenda Alikiba niko naye kwa hiyo kuna sehemu zingine mimi sipo sababu sina sababu ya kuwepo, Alikiba amekuwa ni mtu ambaye hapa nchini hakai sana kwa kipindi hichi ndiyo maana wanakuwa hawaoni tupo pamoja” alisema Baraka The Prince
Mbali na hilo Baraka The Prince amesema kuwa mkali huyo wa Aje hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya kuachia kazi yake mpya baada ya Aje kusumbua zaidi ya mwaka mzima.
Alikiba na Baraka The Prince licha ya kuwa chini la label moja ya RockStar4000 wasanii hao pia waliachia kazi ya pamoja ambayo inafahamika kama ‘Nisamehe’