-->

Aika: Mnaosubiri Niolewe na Nahreel Mtasubiri Sana

BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa mwanadada Aika Mariale na mpenzi wake wa siku nyingi, Nahreel, wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Navy Kenzo, wapo kwenye mipango ya ndoa, mwanadada huyo amefunguka kuwa hakuna kitu kama hicho kwa sasa.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Aika wa nahreel alisema watu  wanapenda kuzusha mambo wasiyoyajua na suala hilo halipo kabisa wala hakuna anayewaza kitu hicho kwa sasa zaidi ya kufikiria jinsi ya kuandaa kazi nzuri za kuwakata kiu mashabiki wao.

“Suala la mimi kuolewa watu watasubiri sana maana hata mipango hiyo haipo kabisa nashindwa hata kulizungumzia, ndoa yetu si leo wala kesho kama ikifika wakati mambo yakiwa tayari tutaweka wazi ila ni huko baadaye sana,” alisema Aika.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364