Gabo Zigamba ni kirusi kwenye tasnia ya filamu – Duma wa Siri ya Mtungi
Msanii wa filamu aliyewahi kufanya vizuri na tamthilia ya Siri ya Mtungi, Duma, amefunguka kwa kudai kuwa muigizaji bora wa filamu 2016 kupitia tuzo za EATV Awards, Gabo Zigamba ni kirusi katika tasnia ya filamu.
Duma amedai muigizaji huyo hawezi kuvaa vizuri na kujiweka kistaa hali ambayo inachafua tasnia ya filamu.
“Gabo ni kirusi, popote alipo anajijua yeye ni kirusi,” Duma aliimbia Global TV. “Lazima ajirekebishe lazima abadilike, Gabo hajafanya kitu chochote toka amepewa tuzo, hata kwenye matukio makubwa hawezi kutokea kwasababu hata akialikwa haonekani kama ni staa. Mtu kama yule anaweza kurudia suti mara tatu kwenye event kweli?,”
Aliongeza,”Mimi nafanya kazi, Gabo ni kirusi kwenye tasnia ya filamu. Kwahiyo kama anataka kubadilika abadilike kwasababu huwezi kuwa staa halafu unaishi maisha sawa na watu wa kawaida,”
Muigizaji huyo amedai yeye ni ‘anti Virus’ hivyo atajitahidi kurekebisha hali hiyo na kuwa mfano kwa wasanii wa filamu.
Bongo5