-->

Aje Ilikuwa Suprise kwa Wema Sepetu – Alikiba

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Alikiba almesema wimbo huo hajamuimbia Jokate na wala hajawahi kumuimbia mtu yeyote, bali aliimba kwa ajili ya mashabiki wake.

kiba233

” Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu”,.

Lakini pia Alikiba alisema kuwa kitendo cha kuwataja wasanii wa Filamu Wema Sepetu na Lulu kwenye wimbo huo, ilikuwa ni suprise, hivyo wenyewe hawakujua kuwa wameimbwa, isipokuwa alishawahi kumdokeza Wema Sepetu ambaye ametaja kuwa ni rafiki yake mkubwa.

“Wenyewe walikuwa hawajui kuwa nimewaimba, ila Wema nilimwambia siku moja kuwa bichwa nina suprise yako, ila Lulu sikuwahi kumwambia na hata sijui ameipokeaje, ila naamini kaipokea fresh”, alisema Alikiba.

Kitu ambacho bado kinawapa kigugumizi watu ambao walikuwa wakifuatilia kipindi hicho, pale aliposhindwa kuchagua kati ya Wema Sepetu na Jokate, na kusema anawachagua wote, na kuzidi kuweka hali ya sintofahamu kwa wawili hawa (KIba na Jokate) huenda bado wako pamoja.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364