Akaunti ya Shamsa Ford Yenye Followers 2.1m Yadukuliwa (Hacked)
Wizi wa akaunti za mitandao ya kijamii kwa mastaa Bongo bado unaendelea – na sasa ni zamu ya Shamsa Ford kulia.
Akaunti ya mtandao wa Instagram ya muigizaji huyo ambayo ilikuwa na followers milioni 2.1 imedukuliwa (hacked) usiku wa Jumanne hii.
Akiongea na Bongo5, Shamsa amesema kwa sasa bado anaendelea kushughulikia jambo hilo kuhakikisha anairudisha akaunti yake hiyo ambayo ilikuwa ni msaada mkubwa kwake kutangaza kazi zake. Kwa sasa akaunti hiyo inatumika kwa jina @umelikoroga_utalinywa.