Barnaba Afunguka Ukweli Kuhusu Mke Wake
Mkali wa bongo fleva Barnaba Classic amesema yeye na mke wake hawajaachana kama watu wanavyoamini lakini wametofautiana kidogo.
“Kwa sasa siko kwenye maelewano mazuri na mama watoto wangu, siyo kwamba tumeachana au tumetengana sitaki kusema hivyo pia wimbo wangu mpya huu wa Lonely sijamuimbia mtu na hauhusiani na maisha yangu kabisa”. Alisema Barnaba
Aidha msanii huyo amesema hawezi kusema hampendi Mama Steve kwa kuwa wameshakuwa kama ndugu yake kwa kuwa wameishi pamoja kwa takribani miaka 9 kabla ya kutengana.
eatv.tv