Mbasha Avunja Ukimya
Msanii wa muziki wa Injili bongo Emmanuel Mbasha, ameamua kuvunja ukimya juu ya tuhuma alizopewa za kutelekela watoto aliozaa na wanawake wotauti tofauti, na kusema habari hizo hazina ukweli wowote.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Emmanuel Mbasha amesema tuhuma hizo ni uongo na anachukia watu wanaotengeneza habari hizo, kwani yeye haitaji habari za kutunga kupata kiki kwa kuwa yeye sio mwanamuziki wa bongo fleva.
“Sio kweli hivyo vitu ni vya uongo, nakanusha kabisa, hivi kwa nini vitu vingi vinaongelewa vya uongo! alafu mimi sipendi, huu uongo uongo ni vitu vya bongo fleva, mimi sipo kwenye kutafuta kiki wala kuongelea vitu ambavyo havina faida”, amesema Emmanuel Mbasha.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba Emmanuel Mbasha amewazalisha wanawake wawili tofauti na kuwatelekeza, kisha kukimbilia kwa mwanamke mmoja mwenye uwezo mzuri kipesa hapa mjini na kuweka kambi.