-->

AliKiba Mwendo Wake wa Kobe Ila Mambo Yake Barida

Alikiba aka King Kiba ni kati ya wanamuziki wa Africa ambao wanashabikiwa na kuwa na umaarufu wa hali ya juu. Hii yote inatokana na utamu wa sauti aliyojaliwa nayo, na kipaji cha mashairi matamu ambayo kwakweli yamekuwa yakiwaburudisha mashabiki lukuki Duniani. Alikiba ambaye kwasasa yuko chini ya kampuni kubwa ya muziki Duniani Sony Music, anauwezo wa kipekee katika muziki na hii ni bayana wazi maana hata Msanii mkongwe wa muziki Duniani Muamerika R. KELLY alishawahi kumshirikisha kwenye project ya muziki pamoja na wasanii wengine wakali Africa.

Alikiba aka King Kiba

Pengine kipaji hiki cha muziki, ndicho kinachompa confidence Alikiba, na hana wasiwasi wowote uanapoamua kufanya mradi wake ndani ya muziki. Alikiba, wakati wanamuziki wengi wakali hapa Africa wakiwa wanaumiza vichwa vyao ilikuhakikisha wanazizuia nafasi zao kimuziki zishishuke chini, yeye amekuwa hababaiki wala kuonesha dalili za kuogopa kuporomoka kimuziki. Anaishi kama mwanajeshi ama comando wakivita anaye pigana vita pekeyake.

Miezi miwili iliyopita, Alikiba alitengeneza vichwa vya habari, pale alipotupia picha alizozipiga akiwa studio na mkongwe wa muziki Africa Yvonne Chakachaka. Kupitia vichunusi vya mitando vya kijamii, pia legendary huyo wa muziki kutoka Africa Kusini alipigia mstari uhakikisho wa collabo ya pamoja na Alikiba huku akimusifia kwa jinsi alivyobarikiwa na kipaji cha uimbaji pamoja na sauti inayoweza kutoa nyoka pangoni. Lakini hadi sasa, mashabiki bado wako solemba wanangojea collabo hiyo. Huku Alikiba akiwa amefyata mdomo kuhusiana na collabo hiyo, anajua fika kwamba wakati ukifika wimbo huo ni lazima utawasha moto wa ajabu na huuenda ukadumu kwa miaka mingi ijayo. Na hii ndio sababu haswa inayomfanya staa huyu wa Africa kuwa tofauti na wengine kabisa katika tasnia hii ya muziki.

Alikiba aka King Kiba

Mwendo wake huo wa kinyonga, unamfanya kutimiza vitu vyake kwa uhakika. Nahivyo kuwafanya mashabiki wake kwasasa kumuelwa na kumwamini kwasana kinyume na siku za nyuma, ambapo kila mashabiki wake walipomuona amekimya walikuwa na wasiwasi yakuwa huuenda mfale wao akapotea kwenye ramani ya muziki. Nikilipigia mustari jambo hili, ni kwajinsi alivyowapa surprise mashabiki wake na wadau wa muziki Africa, pale jana alipotangaza kuwa kuna bidhaa zenye jina lake ikiwemo jense na vinywaji vya energy vitakavyo ingia sokoni sio mda mrefu. Kwakweli hili hakuna aliyeliona linakuja, ila pengine kwa team yake na watu wake wa karibu tena wasiri sana. Japo mwendo wake niwapolepole, anachokifanya huwa maridhawa na chenye faida kwake na pia hudumu kwa mda mrefu. Kweli mwenda pole huwa hajikwai na akijikwaa huwa haanguki na wakamalizia wakasema akianguka basi haumii.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364