-->

Antu Mandoza Msomi Mwenye Bahati Kuigiza Filamu Kubwa ya Kiumeni

Apania kutwaa Tuzo za Oscar kama Lupita

BONGO movie huwezi kupata bahati ya kuingia moja kwa moja na kupewa thamana kuingiza kama mwigizaji kinara, ni mamisi tu ndio wenye bahati hiyo lakini mwingine lazima asote, kwa Antu Mandoza ‘Miss Mandoza’ mwigizaji kinara katika filamu ya Kiumeni ni tofauti, yeye sinema yake ya kwanza anapewa nafasi ya mhusika mkuu.

Antu mwigizaji wa filamu ya Kiumeni akiwa katika pozi la picha akifurahia jambo

Mandoza ni mtoto wa Kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watu wa Dokta Mandoza, ambayo si familia ya waigizaji yeye anakuwa wa kwanza kuigiza japo siku za nyuma aliwahi kushiriki katika tangazo Bongo star Search fungua njia lilotengenezewa nchini India mwaka 2011, lenye viashiria vya uigizaji.

” Kiumeni ni Filamu yangu ya kwanza kufanya, Sijawahi kuwaza kufanya filamu hapo awali , maigizo niliwahi kushiriki zamani sana primary school but sikuwahi kuchukulia serious au kudhani ningekuja kufanya sanaa katika umri wa ukubwani,”alisema Antu.

Antu Mandoza kitaluma ni mtaalamu wa mawasiliano ya umma (Mass Communication) ana degree ya arts in Mass Communication aliyohitimu katika Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (Mlimani UDSM) baada ya kuhitimu alishiriki katika taasisi mbalimbali katika kufanya nazo kazi.

Aliwezaje kuingia katika tasnia ya filamu na kupata nafasi, anasema kuwa alikuwa na rafiki yake wa karibu ambaye alipoona tangazo la usaili alimushawishi kushiriki katika usaili lakini kilichomvutia zaidi ilikuwa mtayarishaji wa filamu hizo Ernest Napoleon kuzikubali kazi zake kama Going Bongo.

Antu Mandoza mwigizaji wa filamu ya Kiumeni

Aliposhiriki alichaguliwa mwigizaji wa kwanza wa kike ambaye aliweza kutumia vema matumizi ya Muswada (Script reading) na kuvaa uhusika hivyo haikuwa vigumu sana pamoja na kuwa na hofu mtayarishaji alichukua nafasi ya kumpatia mafunzo rasmi ya uigizaji.

“Naishukru team ya Kiumeni I was worried sikuwa najua mengi about kuigiza ila the team waligundua nina Kipaji(i have a talent), Ernest alinifundisha mengi (As in trained me ), Director Nicholaus pia did a very good job kuhakikisha (i did what i had to do) nafanikiwa kuigiza,”

“Nilikua na mashaka na maswali mengi so nilienda tu kama kujifurahisha , waliponifanyia screening na script reading wakaona nafaa (and Here Iam today Female Lead) wa Kiumeni. Kiutani utani,”
Msanii huyo anafurahia kwa sasa kupata salam nyingi za pongezi kwa mwigizaji wa kimataifa kwani tayari amekuwa akipata mialiko mbalimbali ya kimataifa kushiriki filamu kubwa kutoka nje baada ya kufanya vizuri katika filamu Kiumeni.

Anaiomba Serikali yetu ya Tanzania kutoa nafasi kwa sinema na kuipa nafasi sekta ya filamu kwani ameona thamani kubwa kutoka nje akitolea mfano Serikali ya Kenya kuwa watayarishaji walivyoposti trailer ilitoa mwaliko kwa timu nzima ya Kiumeni kwenda Mombasa kufanya Premier.

“Serikali ya Kenya kupitia bodi ya filamu ya Kenya walipoona tu trailer walituita wakati muamko kama huo Tanzania haukuwepo, na so far hata request za kazi nilizopata kazi ni kutoka Kenya.

wanajivunia mno Kiswahili na wako very supportive kwa wasanii wao kwa ujumla,” alisema Antu.
Wakati kwa serikali yetu hapa iliona kama kitu cha kawaida tu lakini anaamini kama tasnia ya filamu itapewa nafasi kisera ni chombo muhimu sana katika utangazaji wa utalii na mali asili nchini, na inaweza kuokoa mamilioni ya matangazo ambayo ufanywa na bodi ya Utalii.

Siku za nyuma Antu aliwahi kujihusha na siasa kidatu cha sita aliwahi kugombea nafasi ya Ubunge viti maalum vijana kupitia CCM Mkoa wa Kagera lakini kura hazikutosha, amekuwa miongoni mwa Raia wenye Uzalendo na nchi yake.

Mara nyingi huchangia katika mijadala ya madawati mbalimbali yenye kujenga na kuleta mtazamo chanya kwa Watanzania hasa vijana wenzake huku akitoa nafasi kwa wanawake ili wapate jukwaa pana katika mijadala inayoweza kuwapa fursa kutoa maoni yao.

Kazi siku za nyuma kabla ya kuigiza
Mwigizaji huyo ambaye anasema katika vitu ambavyo hapendi ni kuwa mtu maarufu hivyo akiwa Clouds Media alikuwa mtayarishaji na mtangazaji wa Kipindi cha So so fresh kilichokuwa kikiruka katika redio ya Clouds fm lakini wanamkumbuka ni wale aliowahi kufanya nao kazi kwa karibu.

Anasema akiwa hapo aliweza kuzalisha vipaji vya wasanii kama Young Killer , Neylee, na wengine kama Rubby, wasanii hao yeye ndio aliweza kuibua vipaji vyao kupitia Fiesta Super nyota ambao hadi leo wanafanya vizuri kwenye fani ya muziki wa Bongo Fleva.

Pia anajishughulisha na shughuli mbali mbali za kijamii kama kuandaa matamasha na kuhamasisha vijana na wanawake katika kujikwamua katika dimbwi la umaskini kwa kutumia fursa zinazowazunguka kwa sasa anafanya kazi Afyacall kama afisa mawasiliano.

Mwisho anaiomba Serikali ya awamu ya tano kusapoti sanaa ya uigizaji na kuithamini kama inavyothamini muziki na Mpira ni rahisi hata kuitangaza nchi upande wa Utalii (Tourism) na vivutio vyetu kupitia filamu, makampuni pia binafsi wasisite kuwekeza kwenye filamu za Tanzania kwani inaweza kuwa biashara na kuwarudishia faida.

Nyota wa filamu ya Kiumeni akiwa katika pozi Antu

Kukuza kazi za sanaa za Tanzania na zaidi na kutangaza utamaduni wa Kitanzania itakayoambata na kukuza Lugha ya Kiswahili yenye waongeaji zaidi ya millioni 200kwa sasa Duniani kote.

Kwa upande wa Mahusiano anasemaje?
Antu Mandoza anasema kwake bado hajawahi kupata changamoto kuhusu kuwa na mpenzi ambaye anaweza kupingana na ndoto zake katika kuitumikia jamii na hata pamoja na changamoto ambazo wasanii upata kutoka kwa wenzi wao kuwazuia haijatokea.

“Nasali kila siku Mungu (I pray that for God) anipe utashi kupata mtu atakayekua mume wangu/mwenza wangu aone hii kazi haina shida, anipe support,”

Kwani matarajio yake kwenye uigizaji ni kufika mbali zaidi kama yalivyo mataraji ya waigizaji wengine kufanya kazi nje ya mipaka ya Tanzania lakini upande wake ana vigezo na malengo mapana zaidi , uchaguzi wa kufanya kazi na mtu au kampuni utategemea sana ubora wa kazi.

Anaangalia kampuni yenye uwezo wa kufanya kazi mbinu na maudhui ya kazi yenye kwa kutumia makampuni makubwa kama Afrika ya Kusini na nje kwani ndoto zake kuwa kama Lupita Nyongo wa Kenya amewezaje na yeye ashindwe kufikia huko?

“Tunataka Lupita mwingine atoke Tanzania kwani mtaji wetu wa Lugha ya Kiswahili tukitumia vema milango ipo wazi kufika mbali zaidi hapa bado tu mwanzo kabisa,”alisema Antu Mandoza.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364