-->

VIDEO:Young Dee: Sijatelekeza Mtoto Wangu

Msanii Young Dee a.k.a Pakarasta amesema yeye hawezi kulea mtoto wake na wala hajui ulezi na ndiyo maana mtoto wake amempeleka kwa mama yake ili aweze kupata malezi mazuri na misingi ya kiimani zaidi.

Young Dee a.k.a Pakarasta

Young Dee amebainisha hayo baada ya kuenea kwa taarifa mbalimbali kutoka katika mitandaoni ya kijamii ambazo zilikuwa zikidai msanii huyo amemtelekeza mtoto wake pamoja na mzazi mwenzake.

“Mimi sijui kulea, sijui ulezi..Mimi mwenyewe nimelelewa.. No mimi mtoto wangu yupo nyumbani, yupo na mama yangu kabisa labda kama nimemtelekeza yeye lakini mtoto yupo salama kabisa…Na yeye mwenyewe sijamtelekeza kabisa kwa sababu ni mzazi mwenzangu  labda kama yeye anasema hivyo kitu ambacho sijawahi sema chochote labda iniradhimu kusema ikiwa imefikia katika ‘pointi’ ya kusema…Nimeamua kumchukua ili mwanagu aweze kupata misingi ya kiimani ya misingi ya  Kimungu kama niliyoyapata mimi”. Alisema Young Dee

Aidha, msanii huyo amedai hajampokonya mtoto mzazi mwenzake kama baadhi ya watu wanavyokalilishwa kupitia mitandao ya jamii ila anachokifahamu yeye kuwa mtoto pamoja na mama yeke wapo nyumbani kwao ili waweze kupata huduma zinazostahiki na kwa wakati

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364