-->

Kajala Afunguka Kupagwa Baada ya Kuhongwa Gari

Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja ambaye kwa sasa yupo karibu sana na msanii Quick Racka amefunguka na kusema kuwa alikurupuka kukubaliana na mwanaume ambaye hakuweza kumfahamu vizuri tabia zake baada ya yeye kuhongwa gari aina ya Harrier.

kajala8322

Kajala alitoa ushuhuda huo kwenye kipindi cha Friday Night Live ya (EATV) alipokuwa akiwapa hamasa mabinti na wasichana kutokukurupuka kwa kuangalia mali za wanaume bali wanapaswa kujisomea ili baadaye waje kuwa na maisha yao wenyewe, kwani yeye alikurupuka na kuolewa na matokeo yake aliishia kufungwa gerezani kwa sababu ya mwanaume wake.

“Ni kweli mfano mimi nilihongwa gari aina ya Harrier nikajikuta nakubaliana na mwanaume lakini baadaye nilikuja kujuta maana niliishia gerezani, hivyo nawaomba mabinti wenzangu tusikurupuke kwenye maamuzi, na wale wasichana ambao wanasoma wanapaswa kusoma ili baadaye waje kuwa na maisha ya kwao wenyewe” alisema Kajala

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364