-->

Amanda Hatishiki na Maneno ya Watu Haumwi ni Mazoezi Tu!

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Amanda Poshi amefunguka kwa kusema yupo salama kabisa kiafya wala hana tatizo lolote kutokana na muonekano wake kupungua kwake kutokana na mazoezi anayofanya kwa ajili ya afya yake anashangaa wale ambao wanamshangaa kupungua mwili wake.

Amanda akiwa katika pozi kwa ofisi.

“Sitishiki na maneno ya wabaya wangu ambao wanahangaika kusambaza maneno na kunishangaa kwanini nimepungua mimi ndio najua kuhusu afya yangu nafanya mazozezi kila siku kwa afya yangu,”alisema Amanda.

Msanii huyo anasema hana sababu ya kumfurahisha yoyote kwa muonekano wake ni yeye anavyoamua kuonekana na si mtu ndio ampangie awe binafsi aliamua kufanya mazoezi kutokana na uzito wa mwili wake kuwa mkubwa sana na kushauriwa kiafya si vema kujiachia na kuwa bonge.

Mwanadada huyo ambaye anamiliki saluni iliyopo mitaa ya Mwananyamala Koma koma anasema watu wamekuwa mabingwa kuwanyooshea vidole watu bila kujua ni uamzi wa mtu kuamua kuwa bonge au mwembamba, siku kila mtu anatakiwa afanye mazoezi kwa nguvu kulingana maradhi kuwa mengi.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364