P Funk Majani Amfunguka Haya Tena Kuhusu Fid Q
Mtayarishaji Mkongwe wa bongo fleva, P Funk Majani amemmwagia sifa rappa Fid Q na kusema kwamba ndiye msanii bora wa siku zote kwa kuwa ni mtu mwenye misimamo na hajawahi kubadilika kufuata upepo wa muziki bali amesimamia misingi ya hip hop.
Majani amemwaga sifa hizo kwenye heshima ya Planet Bongo ya East Africa radio, Ijumaa hii na kusema kwamba hawezi kubadili kauli yake ya kwamba Fid Q ndio msanii bora wa hip hop na kusisitiza ubunifu na upekee alionao rapa huyo kutoka jiji la Mwanza ndio sababu kubwa inayomfanya aendelee kusimamia msimamo wake.
“Muziki ni beat lakini pia ni mashairi. Unapozungumzia msanii, Fid Q ni ‘full package’ kwa sababu ni mbunifu, na mashairi anayo ya ktosha, haigii msanii yoyote kutoka nje lakini hajawahi kubadilika kutokana na upepo wa game. Kila mara unapomuona Fid utaona kuna vitu vinaongezeka kwake lakini vya kipekee kabisa. Kuna wasanii wanaofanya vizuri lakini ukisikiliza mashairi yao huelewi ila Fid licha ya kuwa na ladha nzuri ya sauti ya muziki lakini mashairi yake yatakufanya useme huyu ni msanii Full Package”– Majani alifunguka.
Kwa upande mwingine Majani amesema wasanii wengi wa hip hop wamekimbilia kuwaiga wasanii wa nje mpaka kushindwa kujitofautisha nao kitu ambacho kinawapotezea ubora sokoni.