Amber Lulu Mtu Wangu – Harmorapa
Msanii Harmorapa amefunguka na kusema hakumlipa Amber Lulu ili wapige picha bali walikuwa pamoja sehemu ambapo matukio hayo yalitokea kwa kuwa wao ni watu wa karibu sana.
Harmorapa anasema kuwa hakuwa na sababu ya kumlipa msanii huyo kwa kuwa wao ni wapenzi , hivyo walipiga hizo picha wakiwa katika mambo yao ya kawaida yanayowakutanisha.
“Amber Lulu mimi sijamlipa kwanza na wala sikumtafuta ili kutengeneza kiki, bali nilikutana naye katika mazingira tofauti, mimi Amber Lulu ni mtu wangu (mpenzi wangu)” alisema Harmorapa
eatv.tv