-->

Apigwa Risasi Nje ya Kanisa Kibangu

Mkazi wa Ubungo, Kibangu amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi wakati akitaka kuingia katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Kibangu, wilayani Ubungo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Akisimulia tukio hilo, mfanyakazi wa kanisa hilo, George Ng’atigwa amesema aliyejeruhiwa ni muumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la Adrian Mpande.

Amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi wakati muumini huyo alikuwa nje ya kanisa akisubiri muda ufike ili aingie kanisani.

“Mara akatokea mtu mwenye bastora akampiga risasi ubavuni na mkononi akaanguka na kuzimia,” amesema.

Amesema baada ya kutekeleza unyama huo, mtu huyo ambaye alifika kanisani hapo akitembea kwa miguu, alikimbia.

Amesema watu waliokaribu na kanisa hilo walimfukuza huku wakipiga mayowe na baada ya muda mfupi alikamatwa.

“Inaonekana alikamatwa baada ya bastora yake kuishiwa risasi kwa kuwa wakati anakimbia hakuwa akiwatishia waliokuwa wakimfukuza,”amesema.

Amesema baada ya kukamatwa,walifanya mawasiliano na Polisi ambao walifika baada ya muda mfupi na kuondoka naye.

Alisema alijeruhiwa kwa risasi alipata huduma ya kwanza katika zahanati iliyopo jirani na kanisa hilo na baadaye kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akifafanua, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kaganda alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba huo ni ugomvi wa kifamilia.

“Mtuhumiwa tunaye tunaendelea kumhoji na aliyepigwa risasi anaendelea vizuri na Matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” amesema.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364