-->

Aunt Ezekiel: Sitaki Marafiki Tena

BAADA ya urafiki wa waigizaji mashuhuri na wanaozungumzwa sana nchini, Wema Sepetu na Aunty Ezekiel ‘Mama Cookie’ kuvunjika, waigizaji hao wameibuka na kudai kwamba hawahitaji marafiki.

wema instagram

ema Sepetu na Aunty Ezekiel ‘Mama Cookie

Ilishangaza Aunty Ezekiel kutomualika Wema Sepetu katika sherehe ya mtoto wake na mnenguaji wa Diamond Platinum, Moses Iyobo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa Serena Hotel.

Aunty Ezekiel alipoulizwa kuhusu urafiki wake na Wema, alisema hataki marafiki kwa kuwa hawamsaidii chochote hivyo kwa sasa rafiki yake mkubwa wa kufa na kuzikana ni mwanae tu.

“Rafiki yangu aliyebaki ni mtoto wangu ambaye atakuwa rafiki wa kufa na kuzikana, Aunty Ezekiel wa kipindi kile si wa sasa, kwa sasa  nimeongezea jina naitwa ‘Mama Cookie’ naishi maisha mengine, nawaza kumlea mwanangu muda wote sina muda na marafiki wengine,” alisema Aunty Ezekiel.

Aunt Ezekiel aliongeza kwamba Iyobo na Cookie ndiyo wanaompa furaha na ndiyo wamebaki kama baba na mama yake.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364