-->

Aunt: Sasa Natafuta Mapacha

STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa baada ya mtoto wake, Cookie kutimiza mwaka, sasa anafanya mpango kutafuta njia ya kupata watoto mapacha ili atulie.
aunt67
Akizungumza na Amani Aunt ambaye amezaa na dansa wa staa wa Bongo Fleva, Diamond, Moze Iyobo alisema kuwa, anamshukuru Mungu kumpa mtoto ambaye amemfungulia njia lakini kwa sasa anatamani mapacha ili awe na jumla ya watoto watatu kisha ndiyo apumzike aendelee na mambo mengine.

“Baada ya Cookie kunifungulia jina la kuwa mama sasa nataka niongeze uzao mmoja wa pacha ili niwe na watatu kisha nitapumzika,” alisema Aunt.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364