-->

Matamasha ya Ngwair, Mama Yake Akumbukwe- TID

Msanii TID ametoa baraka kwa mtu yeyote anayetaka kufanya kitu chochote ikiwemo matamasha ya kukumbuka kifo cha msanii Albert Mangwea na kuenzi kazi zake kufanya hivyo, ila ni lazima wahakikishe wanapata kibali kutoka kwa mama mzazi wa Mangwea.

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

Muimbaji wa Bongo Fleva TID akiwa na rapper KR Mullah

Akiongea na ENews ya EATV TID amesema hawezi kumzuia mtu kufanya hivyo kwani ni kitu kizuri, isipokuwa ni lazima wahakikishe kiasi kinachopatikana lazima asilimia kadhaa ziende kwa mama mzazi wa Ngwea.

“Nawapa blessing mtu yeyote anataka kufanya memorial ya Ngwear, mi nampa go ahead ila awasiliane na mama, na chochote kitakachoingia lazima percentage iende kwa mama, mama mzazi wa Mangwea”, alisema TID.

TID amesema amefikia hatua ya kusema hayo ili watu wasijinufaishe na kifo chake, na kutoa taarifa kuwa wameandaa project na foundation maalum ya kuenzi kazi za Ngwea, na tamasha litakalofanyika siku ya Jumamosi wikii hii.

“Sisi kama Radar tumeandaa project maalum, pia kutakuwa na foundation kwa ajili ya kuenzi kazi zake na watu kumjua Ngwea, pia kutakuwa na Tamasha na watu kibao ambao tumewaalika, itakuwa Albert Magwer foundation tribute to his music” , alisema TID.

TID aliendelea kwa kusema kuwa ana imani kuwa mama mzazi wa msanii huyo anafaidika kwa kazi za mwanaye, kwani mikataba iliyosainiwa aliwekwa kama mrithi wa mali zake.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364