Baada ya Kusugua Benchi Miaka Mitano, Nora Afunguka
STAA aliyekuwa akitingisha kwa wasanii Bongo kutoka Kundi la Kaole, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa Mungu amemuona baada ya kukaa benchi kwa takriban miaka mitano bila kurekodi sinema.
Akizungumza na Ubuyu wa Town, Nora alisema alikuwa ameshakata tamaa lakini anaishukuru Kampuni ya Didas Entertainment ambayo imemthamini na kumrudisha tena kwenye gemu.
“Watu waliniona mimi sifai tena wala sina thamani tena lakini Dida aliniona mimi nina kipaji cha pekee, amenichukua na kufufua kipaji changu cha enzi na enzi, soon mashabiki wataniona,” alisema Nora.
Chanzo: GPL