-->

Baada ya Miaka Sita Lady Jaydee Akutana na Ray C

Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Ndi Ndi Ndi’ Lady Jaydee amekutana na msanii Ray C baada ya miaka sita. Baada ya kuonana Lady Jaydee alisema kila mtu anapitia magumu katika maisha kwa njia tofauti.

Jide

“Kila mtu anapitia magumu katika maisha kwa njia tofauti hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea, amini na amua nakupa moyo na Mungu akusaidie kwa yote unayopitia akuondolee akuepushie na akupe kufahamu na kukiri mabaya” aliandika Lady Jaydee

Lady Jaydee aliendelea kumtia moyo msanii huyo na kumwambia kuwa kwa sasa anakumbuka ule ushindani waliokuwa nao kipindi cha nyuma kwenye muziki na kumweleza kuwa arudi tena kwani bado ana nafasi ya kuweza kufanya vizuri.

“Nakumbuka tulivyo anza kimtindo nai miss ‘competition’ tafadhali rudi tena naamini bado unayo nafasi. Binti amka jikaze anza mwendo umrembo na bado wang’ara. Ni baada ya miaka 6 tangu kuonana mara ya mwisho story nazo ni ndefu na nyingi”. Aliandika Lady Jaydee

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364