-->

Baba Haji Akomalia Sinema za Kidini

MUIGIZAJI mkongwe Bongo, Haji Adam ‘Baba Haji’, amesema baada ya kucheza kwa mafanikio filamu ya Ndoto Bayana, ambayo ina maudhui ya dini ya Kikristo, sasa anakusudia kufanya kazi nyingine kama hiyo, lakini kwa Kiislamu.

baba-haji-2

“Nimejikuta nikipata wazo kuwa naweza nikafanya kazi hizi za kidini na bado nikawa nipo sokoni kama kawaida, kitu kingine kilichonivutia filamu hizi ni kuwa licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, lakini pia zinafundisha sana. Nadhani ni muda muafaka wa kubadilika,” alisema.

Akiizungumzia filamu hiyo, Baba Haji alisema inazungumzia ndoto iliyokuwa ikiotwa na mkewe, ikiashiria ujio wa tukio la kishirikina, ambalo lilishindwa kutokana na nguvu ya maombi. Wengine walioshiriki filamu hiyo ni Thea, Patcho Mwamba na ‘mkewe’ Maureen Kunambi ‘Hakiki’.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364