-->

BABA HAJI: Bila Haya Tasnia ya Filamu Itayumba

Mwigizaji Haji ‘Baba Haji’ Adam amesema soko la filamu lipo isipokuwa limekosa msisimuko kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo baadhi ya wasanii kukosa ubunifu na kutunga kazi zisizokuwa na ubora. Kauli hiyo ya Baba Haji inatofautiana na za baadhi ya wasanii wenzake ambao wamekuwa wakilalamikia kukosekana kwa soko hilo huku wakitaja sababu kadhaa.

Baba Haji

Baba Haji

Anazitaja baadhi ya sababu zinazochangia kukosekana kwa msisimko huo kuwa ni wasanii kutunga bora liende, kutumia CD yenye filamu kufanyia matangazo ya filamu ijayo, hivyo kuwa na wateja wale wale ambao wametizama filamu hiyo tofauti na tangazo likirushwa katika vyombo vya habari litaangaliwa na wengi na kuongeza watazamaji wapya.

“Siyo lazima kila mwigizaji awe mtunzi, tunaweza kuwa na waigizaji na watunzi na wakafanya kazi pamoja na zikawa za kuvutia.

“Nakumbuka siku za nyuma kulikuwa na watunzi tofauti na waigizaji, lakini sasa mtunzi, mtayarishaji, mwongozaji, mwigizaji anaweza kuwa mmoja katika filamu nne hadi tano, bila shaka atachoka na kufanyia mazoea, ”anasema Haji.

Haji anaongeza kuwa hilo limelalamikiwa muda mrefu lakini limekosa ufumbuzi kwa kisingizo cha mitaji midogo, hivyo siyo ajabu kukosekana msisimko kwa kinachoendelea.

Anasema tasnia ya filamu imetoa ajira kwa vijana wengi na inaendelea kutoa huku ikibadili maisha yao kwa ujumla, hivyo kuna haja wawekezaji wakawekeza na huko ili kuiinua na kuirudisha katika hadhi yake.

Anaeleza kuwa iwapo kutakuwa na wawekezaji, kutakuwa na ushindani wa kweli ambao utaleta tija bila kufanya hivyo itabaki hadithi, malalamiko lakini ukweli ubaki pale pale mitaji midogo.

Anazitaja sababu za kutoa kuwa kwa mitaji ya waigizaji licha ya kuigiza miaka nenda rudi kuwa ni kilio kile kile cha wizi wa kazi zao. “Sidhani kama kuna mwigizaji aliyewahi kulipwa zaidi ya mara moja, hata kama filamu kali kiasi gani utakachopata ni malipo ya awali siyo kama watu wa vitabu ambao huitwa vinapotaka kutolewa kopi ya mara ya pili na kuendelea, filamu ikitoka siku ya kwanza ya pili zimejaa mitaani.

“Kibaya zaidi kutokana na kuwa mwezeshaji mmoja au wawili, kila filamu inayoigizwa siyo yetu, hivyo ikiwa mikononi mwa muhusika anafanya anachotaka bila kukushirikisha ilimradi alikulipa chako hata kama ni kidogo, kama hakuna uwekezaji wa kweli, kukuza mitaji sekta ya filamu itabaki historia, ”anasema Haji.

Haji anamuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, wasanii na Michezo, Nape Nnauye kuiangalia mara mbili sekta hiyo kwa kuhakikisha kunakuwa na haki miliki na hati bunifu.

Anasema hatua ambayo aliianza Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, hivyo siyo vibaya waziri aliyeteuliwa na Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kuiendeleza.

Chanzo: Mwananchi

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364