-->

Baby Madaha: Nimeamua Kutulia na Ndoa Yangu ya Kiarabu

MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Baby Joseph Madaha, ameibuka na kudai kwa sasa ameamua kutulia katika ndoa yake na Mwarabu wa Dubai ambaye hakutaka kumtaja jina.

Baby Madaha

Baby Madaha

Baby yupo mbioni kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Corazon’ unaofanyiwa video yake nchini Dubai kwenye makazi yake mengine.

“Kwa sasa ninaishi nchi mbili, nipo Tanzania na pia nina makazi yangu mapya huko Dubai, nimeolewa na Mwarabu na nimetulia kwenye ndoa yangu najiachia kwangu, ahaaaa!” alijibu kisha akamalizia kwa kicheko.

Akizungumzia wimbo huo, Madaha alisema ameurekodia katika studio za C9 zinazomilikiwa na prodyuza mkali katika midundo nchini, Christopher Kanjenje (C9).

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364