-->

Nay Wa Mitego Afungukia Vitisho Alivyovipata Kwenye ‘Salaam Zao’

Mkali wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka kuwa ingawa  asilimia kubwa ya ngoma zake zinazofanya vizuri ni zile ambazo inaonekana amediss watu live kwa kuwataja majina lakini katika maisha yake anasema hatoisahau wimbo wa Salaam Zao kwa sababu ndiyo wimbo iliyowahi kumpa shida kuliko nyimbo zake zote.

nay987

‘’Ngoma ya Salam Zao nilipokea vitisho vingi sana,kwasababu kwanza nakumbuka kuna mmoja kati ya watu niliowataja alishawalipa mawakili na mmoja kati ya hao mawakili alikuwa ni shabiki wangu akaniambia mpaka muda huo kuna mawakili kama watatu wameshalipwa hela natakiwa kwenda mahakamani akaniambia nijipange kama nina wakili nijiandae kwenda mahakamani’’ Alisema Nay Wa Mitego.

‘’Yule wakili alinihakikishia kwa kitu ambacho nimeimba wao walikuwa wakifanya vile kwasababu wamelipwa nikiwa na wakili mzuri nilikuwa sina kesi,iliniletea shida sana lakini kwasababu huwa najua ni kitu gani nafanya na kabla sijaimba huwa nafanya uchunguzi kwahiyo huwa najipanga kabisa litakalonitokea baada ya ngoma kutoka’’ Aliongeza Nay Wa Mitego.

cloudsfm

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364