Bado Nipo Kwenye ‘Game’ – Soggy
Mwana hip hop ambaye amewahi kuishika game ya bongo fleva miaka ya nyuma, Soggy Doggy Hunter, amesema hajaacha muziki, licha ya kutosikika akitoa kazi mpya kwa kipindi kirefu.
Soggy amewatoa shaka wapenzi wa bongo fleva, alipokuwa akizungumza na EATV, ambapo amedai kuwa kila siku anaandika ngoma ngoma mpya na kwamba hadi sasa ana ngoma zaidi ya 16 alizokwisha rekodi, lakini hajaziachia kwa kuwa bado anausoma mchezo.
“Siwezo kuacha muziki bro, hapa nilipo ni kama ngoma 16 hivi, zipo tu, utazisikia muda si mrefu” amesema.
Kuhusu uwezekano kubadili aina ya muziki ili kuendana na soko, Soggy amesema kuwa anaendelea na mtindo ule ule kwa kuwa yeye ni mwana hip hop
“Siwezi kuimba wala kufanya singeli, naendelea na hip hop kama kawaida” Amesema Soggy
Soggy amewahi kutamba na ngoma kama vile ‘kibanda cha simu’ na ‘nilikaona mwaka jana’ kabla ya kuwa kimya kwenye muziki.
eatv.tv